HISTORIA YA MWONGOZO WA IR-VICOBA
Chimbuko
la mwongozo wa IR-VICOBA ni mkutano wa wadau wa VICOBA vya waumini wa dini
mbalimbali uliofanyika mjini morogoro mwezi mach 2010. Wadau hawa walikutana
mjini morogoro kujadili maendeleo ya utekelezaji wa mpango wa uendeshaji wa
VICOBA vilivoanzishwa kwa juhudi za taasisi za dini mbalimbali na baadhi ya
mashirika ya dini. Kutokana na changamoto zilizojadiliwa katika ngazi mbalimbli
wadau walikubaliana kurejea kitini cha mwongozo cha mpango wa VICOBA cha 2008
chaWCRP. Baada ya maboresho hayo ambayo yamejibu mapungufu yaliyokuwepo awali,
dini mbalimbali zilitoa mwongozo wa kufundishia na uendeshaji wa vikundi
vilivyo chini yao, yaani IR-VICOBA.
Neno
VICOBA ni kifupisho cha ‘Village Community Banks’ Mpango wa VICOBA ulianzishwa
mwaka1991 katika nchi ya Niger Na shirika la kimataifa la CARE. Niger katika
wilaya ya Maradu ukijulikana kwa jina Mata Masu Dubara (MMD)
MMD
ilihamasisha vikundi vya akiba na mikopo kwa mfumo wa upatu wa asili
ulioboreshwa ambao kwa Tanzania unaitwa VICOBA Fedha zinazo wekezwa kwenye
kikundi hutumika kuwakopesha wanachama kwa ajili ya kuendeshea shughuli
mbalimbali za kiuchumi.
Mfumo
wa MMD uliingia Tanzania visiwani katika eneo la Jozan mwaka 2000 na kuitwa
Jozani Savings and Credits Association (JOSACA). Mwaka 2002 WCRP(World
Conference of Religions for peace) Tanzania walianzisha mpango huu kwa
majaribio katika kata ya ukonga, wilaya ya Temeke, Mkoa wa Dar es salaam na
wilaya ya kisarawe mkoa wa pwani kwa mara ya kwanza mpango uliitwa Village Community
Banks (VICOBA) na WCRP Tanzania baada ya kujifunza mfumo wa JOSACA Zanzibar.
Mfumo
huu kwa Tanzania unajulikana kwa majina mengi kama COCOBA, SILK Tanzania, VICOBA,
na JOSACA. Kwa Tanzania tayari mfumo huu umeweza kufika katika mikoa ya Dar es
salaam, pwani, Tanga, Arusha, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Kigoma, Shinyanga, Mwanza,
Mtwara, Singida, Manyara, Dodoma na Njombe, Mtwara na Geita kwa kupitia
mashirika yanayo tekeleza shughuli mbalimbali za kuinua kipato cha mwananchi.
Kuanzia
mwaka 2007, taasisi za dini zilianza kutoa mafunzo kuendesha na kuunda vikundi
vya VICOBA kwa ufadhili wa shirika la Norwegian Church Aid (NCA) Tanzania ili
kutofautisha kati ya vikundi hivi na vikundi vinavoanzishwa na taasisi nyingine
ndio maana vikundi vyote vilivoanzishwa na taasisi za dini vinaitwa ‘Inter
Religious VICOBA (IR-VICOBA).
Pongezi kwa; CCT (Christian Council
Tanzania), TEC (Tanzania Episcopal Conference), BAKWATA (Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania), ELCT’S (Evangelical Lutheran Church in Tanzania), IRCPT (Inter Religious
Council for Peace in Tanzania), AEE-T (African Evangelistic Enterprise
-Tanzania)
Facebook Blogger Plugin by Tanzaniastar
Chapisha Maoni