Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Kampeni ya kupambana na kipindupindu kilichoikumba wilaya ya Kilosa, imeendelea kwa siku ya jana katika kijiji cha Mabula, hichi kijiji kina historia ya kukumbwa na kipindupindu.

Imeonesha kua wananchi wa eneo hilo wanatumia maji ya mto na hawana desturi ya kuchemsha maji ya kunywa wala kuyatibu, Pia wananchi wengi hawana vyoo bora na wengine kutokua navyo kabsa hii ikapelekea serikali kupitia mtendaji wa kata kuweka tamko la mtu asiyekua na choo bora akamatwe na kupigwa faini ya sh 50,000/=, pia wamekua wakilalamika kukumbwa na malaria mara kwa mara yote hii ni kwa sababu, wanachimba madimbwi kwenye mto uliopungua maji, unaowazunguka na kuyaacha ambapo inapelekea mazalia ya mbu.


watoto wa kijiji cha mabula wakifundishwa jinsi ya kutumia kibuyu mchirizi


Mtendaji wa kata akihamasisha wananchi kua na vyoo bora kuepuka magonjwa ya kuhata na kipindupinduu kisiingie kwenye kata hiyo.



Bonza Mshana toka wizara ya afya (kibaha) akitoa elimu ya afya kwa wananchi wa mabula

Hiki choo kimekosa sifa 3 kua choo bora
1. hakina paa
2. hakina mlango
3.hakina bomba la kutolea hewa

Thanks For Visiting, Our Website Come Again For News, Advertisement And Good Articles

Keep This blog site In Your Mobile For More Updates

Facebook Blogger Plugin by Tanzaniastar
https://www.facebook.com/Tanzaniastar
Next
This is the most recent post.
Previous
Taarifa za zamani

Chapisha Maoni

 
Top