Imeonesha kua wananchi wengi wa wilaya ya Kilosa na Gairo hawafuati kanuni za afya bora, ambapo wanakunywa maji bila kuchemsha wala kuyatibu, hawatumii vyoo bora na wengine hawatumii kabisa, moja kwa moja ikapelekea kukumbwa na ugonjwa huo.
Shirika la misaada la norway NCA (Norwegian Church Aid) kupitia kwa afisa miradi ya WASH ndugu Zachayo Mkobero wakishirikiana na ACT dayosisi ya Morogoro pamoja na uongozi wa serikali kuanzia ngazi ya wilaya mpaka vijiji, wamezindua kampeni katika kijiji cha Msowero wilayani Kilosa ambapo ni sehemu mojawapo iliyokumbwa na kipindupindu. Kampeni hii itachukua siku kumi katika wilaya ya Gairo na Kilosa kwa kauli mbiu ya "mazingira safi na maji salama kwa afya bora sote tuungane kuyatunza"
Vijana wa YouthCAN wakitoa elimu ya mazingira na afya kwa njia ya nyimbo
wananchi wa msowero
Facebook Blogger Plugin by Tanzaniastar







Chapisha Maoni