IR-VICOBA Ni mfumo wa kujiwekea akiba kwa mfumo wa hisa, ambapo watu wa imani mbalimbali au dini mbalimbali kuanzia 15-30 huunda kikundi na kukubaliana bei ya hisa na kuanza kuweka akiba zao, pia kikundi kinatakiwa kua na mfuko wa jamii ambapo utawasaidia wanachama/mwanachama pale ambapo atapata matatizo ya afya au ada shuleni km anasoma/somesha na marejesho yake hayana ziada kama ilivo kwa hisa. Baada ya week 13 huanza kukopeshana kwa makubaliano yao wenyewe kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi, mwanachama anaruhusiwa kukopa kiasi kisichozidi mara tatu ya hisa zake. na mwanachama inatakiwa arejeshe baada ya miezi mitatu pamoja na ziada ya huo mkopo aliochukua ili wanachama wengine waendelee kukopa.
Kikundi kinakua na viongozi wafuatao: mwenyekiti, katibu, mweka hazina na wahesabu fedha wawili pia kunatakiwa kua na wajumbe watatu watunza funguo, viongozi watakaa kwa mda wa mwaka mmoja madarakani. viongozi wa dini na serikari hawaruhusiwi kua viongozi wa IR-VICOBA kulingana na nyazifa zao katika jamii.
Kikundi hujitungii sheria zao wenyewe za kujiongoza, kikundi hukubaliana wakati mwafaka wa kukutana.
kwa maelezo na mafundisho zaidi youthcantanzania@gmail.com
Facebook Blogger Plugin by Tanzaniastar







Chapisha Maoni